Nilichukua udhu kwa ajili ya swala, nikambeba mtoto akachafua nguo zangu kwa mkojo, nikaosha sehemu iliyoingia mkojo na nikaswali bila ya kurudia udhu, je swala yangu ni sahihi?
Jawabu:
Swala yako ni sahihi, kwasababu kilichokupata katika mkojo wa mtoto hakichangui udhu. Hakika hakuna vingine inapasa kuosha kile kilichokupata.
Chanzo: Lajinatu Daaima (Kamati ya kudumu ya kutoa fat'wa ya Saudia Arabia)