Je udhu utaharibika kwa kule tu kutazama wanawake au wanaume walio uchi? Na je udhu utaharibika kwa mtu kutazama utupu wake?
Jawabu:
Udhu haubatiliki kwa mwenye udhu kutazama wanawake au wanaume walio uchi wala kujitazama yeye mwenyewe, kwa kutokuwepo dalili ya hilo.
Chanzo: Lajinatu daaima